Thursday 2 June 2016

JAMAA APIGWA FAINI YA TSH MILIONI 4 KWA KUTUMIA SALAMU YA HITLER

images (14)Jamaa mmoja ametozwa faini ya fedha Euro 1,600 sawa na shilingi milioni 4 za Kitanzania kwa kutoa salamu ya ishara ya Hitler mwaka jana wakati wa tamasha la muziki nchini Ujerumani.

Mahakama ya Bochum iliyomtoza faini jamaa huyo pia imetoa hukumu ya adhabu kwa watu wengine wawili wanaodaiwa kumtusi na kumdhalilisha msichana mmoja mweusi wakati wa tamasha.

Mmoja wa watuhumiwa hao amepewa adhabu ya kuhudumia umma kwa muda wa saa 100 huku mwenzie akitozwa faini ya fedha Euro 750.

Maelezo zaidi yanaarifu kwamba nusu ya fedha hizo atalipwa msichana huyo na nusu yake zitapelekwa North Rhine-Westphalia.

clouds stream