Sunday 26 June 2016

Bosi CRDB ‘Amgwaya’ Magufuli, Asema Sio Binadamu Wa Kawaida



Tarehe June 26, 2016Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Charles Kimei.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Charles Kimei.
Katika hali  isiyo ya Kawaida  Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Benki ya CRDB  Dkt Charles  Kimei amewavunja mbavu  wananchi pamoja na viongozi mbalimbali aliposema Rais Dkt. John Pombe Magufuli sio Binadamu  wa kawaida.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa maboresho ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam leo  Dkt. Charles  Kimei amesema amekuwa anaogopa sana kukutana na Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwa anamchukulia kama sio Binadamu  wa kawaida kufuatia kuja na mfumo wa aina yake wa kuongoza nchi kwa kutumbua majipu.
Amesema amekuwa akihofia mambo mawili kukutana na Rais la Magufuli la kwanza ni kubaki salama na la pili ni  kutumbuliwa.
“Rais Magufuli sio Binadamu wa kawaida kwani tangu aingie madarakani nimekuwa nikiogopa sana kukutana naye kwani asije akanitumbua.”Alisema Kimei.
Kauli hiyo ilionekana kuwavunja mbavu wananchi walio hudhuria katika uzinduzi huo akiwemo Rais Dkt.John Pombe Magufuli mwenyewe.
Hata hivyo Rais Magufuli wakati anahutubia alimjibu kiaina kuwa watendaji wanajitumbua wenyewe kutokana na makosa yao.

clouds stream