Thursday 29 January 2015

Majambazi wapiga na kupora bunduki na risasi polisi

Majambazi wapiga na kupora bunduki na risasi polisi


T1
Ikiwa ni wiki moja Tangu polisi kuporwa bunduki na kuuwawa huko Ikwiriri, janga hili limeendelea tena pale watu wanaosadikiwa ni majambazi kuwapiga na kuwapora bunduki na risasi askari huko jijini Tanga. Kwenye tukio hilo lililotokea barabara ya tano huko Tanga baada ya Askari waliokuwa wakitoka kula chipsi kuvamiwa na majambazi na kupata kichapo kikali kabla ya kuamuliwa kuachia Bunduki.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Juma Ndaki amesema katika tukio hilo ambalo askari PC Masoul alichomwa kisu na akapelekwa haraka kwenye hospitali ya mkoa wa Tanga. Pia amesema upelelezi unaendelea ili kubaini watu waliofanya tukio hilo ila mpaka sasa ajapatikana mtu yoyote anaehusika na uporaji huo.

clouds stream