Thursday 29 January 2015

Wahudumu Mochwari wasusia kuzika maiti kisa kutolipwa Mishahara

Wahudumu Mochwari wasusia kuzika maiti kisa kutolipwa Mishahara

Wahudumu wa mochwari kisa kutolipwa mishahara yao.
Wahudumu wa mochwari kisa kutolipwa mishahara yao.
Wahudumu wa Mochwari katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu wamegoma kuzika miili ya watu iliyoharibika kufuatia hospitali hiyo kushindwa kuwalipa mishahara yao.
Aidha, wahudumu hao  ambao  ni  tisa   walisema jana  kuwa  tangu mwezi   juni mwaka jana hadi sasa hawajalipwa mishahara yao licha ya kufikisha madai yao katika uongozi wa hospitali hiyo na halmashauri ya wilaya ya Bariadi.
Wahudumu   hao Walisema  katika  madai  yao, wanaidai hospitali hiyo zaidi ya Sh milioni 2 huku wakibainisha kuwa kila mmoja anadai Sh 260,000 kwa ajili ya malipo ya kazi wanayofanya ya maziko.
Kwa upnde wa  Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Godfrey Mpangala, alikiri kuwapo kwa madai ya wahudumu hao na mgomo huo  na  kubainisha kuwa tatizo lilitokana na Serikali kutopeleka fedha  za  matumizi  mengine  suala  lililopelekea    kushindwa  kuwalipa  wahudumu hao.

clouds stream