Wednesday 21 January 2015

Liverpool,Chelsea zatoka sare


Liverpool,Chelsea zatoka sare



Liverpools-Raheem-Sterlin-011
Raheem Sterling akifunga goli kwa upande wa Liverpool
Majogoo wa jiji Liverpool wameambulia sare kwenye mchezo wa kombe la ligi uliochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Anfield,kwenye mchezo huo ambao ulikuwa ni mkali sana Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kwa njia ya penati baada ya winga wake Eden Hazard kufanyiwa faulo kwenye eneo la hatari na beki Emre Can.Penati hiyo ilifungwa na Hazard kwa kumpeleka kipa upande mwingine na mpira kuingia kwingine.
240AC75800000578-0-image-a-21_1418914380875
Liverpool walishambulia kwa sana lango la Chelsea mpaka winga wake machachari  Raheem Sterling kuipatia timu hiyo goli la kusawazisha kwenye dakika ya 59 ya mchezo. Kwa sare hiyo ya 1-1 kwenye uwanja wa Anfield inaipa nafasi Chelsea kujipanga kwenye mechi ya marudiano kwenye uwanja wa nyumbani Stanford Bridge.

clouds stream