Wednesday 21 January 2015

Somalia:rais apiga marufuku lugha ya kigeni


Somalia:rais apiga marufuku lugha ya kigeni



Rais Hassan Shaykh Mahmud.
Rais Hassan Shaykh Mahmud.
Rais wa Somalia amepiga marufuku ya matumizi ya lugha za kigeni katika ofisi za serikali na kusema kuwa lugha pekee ya mawasiliano katika ofisi hizo ni kisomali.
Aidha, Rais Hassan Shaykh Mahmud alikuwa akizungumza hayo katika sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 42 tangu kuanza kutumika kwa lugha ya Kisomali nchini humo ,maadhimisho yaliyofanywa mjini Mogadishu kwa lengo la kutaka kuiimarisha lugha hiyo.Hata hivyo maadhimisho hayo yalihudhuriwa na mamabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini humo.
Matumizi ya lugha ya kisomali katika ofisi za serikali yametakiwa kuanza January mosi mwaka huu na kuendelea. Shughuli zote za kiserikali nchini humo zimetakiwa kuendeshwa katika lugha ya kisomali na si lugha nyingine yoyote. Ruhusa ya matumizi ya lugha za kigeni imetolewa tu wakati wageni kutoka nje ya somalia watakapo kuwa wakihudumiwa .

clouds stream