Thursday 15 January 2015

Dk Slaa kufunga ushahidi kesi ya utapeli

Dk Slaa kufunga ushahidi kesi ya utapeli 

Dk. Wilbroad Slaa.
Dk. Wilbroad Slaa.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, leo anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Hai kutoa ushahidi katika kesi ya utapeli inayomkabili kijana aliyejifanya Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta. Katika kesi hiyo Dk Slaa anatarajiwa kufunga ushahidi katika kesi hiyo.
Kwa Upande wa mashtaka, ukiongozwa na Wakili wa Takukuru, Susan Kimaro ulidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Aprili na Mei 2012 ambapo hata hivyo  Mtuhumiwa alikana mashtaka hayo .
Katika kesi hiyo Katika ushahidi uliotolewa mahakamani, Dk Slaa akiwa Mtendaji Mkuu wa Chadema, ndiye anayedaiwa kushughulikia suala la mshtakiwa kutaka kuwatapeli viongozi wa Chadema.
Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Hai, Dennis Mpelembwa alisema jana kuwa Dk Slaa amethibitisha kuitikia wito huo wa Mahakama.
Kwa upande mwingine, Jaji Samatta na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wamekwishatoa ushahidi wao katika kesi ambayo  inayoendeshwa na mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

clouds stream