Friday 23 January 2015

Wenger aanza kumtolea macho Paulista

Wenger aanza kumtolea macho Paulista


Mlinzi wa Villareal, Gabriel Paulista Kkushoto akiwania mpira.
Mlinzi wa Villareal, Gabriel Paulista Kkushoto akiwania mpira.
Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, amesema kuwa kilabu yake imeanza mazungumzo na mlinzi wa Villareal Gabriel Paulista.
”Mazungumzo yanaendelea vyema, Hatahivyo sijuia kama tutaafikia makubaliano,lakini tuna fursa ya mafanikio”.
The Gunners italazimika kumtafutia cheti za kufanyia kazi mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 24.
Arsenal imemsajili Krystian Bielik kutoka klabu ya Legia warsaw kwa kitita cha pauni 2.4 wiki hii huku Wenger akisema kuwa Bielik ambaye anaweza kucheza katika safu ya kati atatumiwa kama kiungo wa kati wa ulinzi.

clouds stream