Monday 19 January 2015

Zambia kufanya uchaguzi wa Rais leo


Zambia kufanya uchaguzi wa Rais leo




Wananchi nchini Zambia wanapiga kura leo  kuchagua Rais wa nchi hiyo, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Michael Sata Oktoba mwaka jana.
Chama tawala cha Patrioyoc Front kina  uhakika wa kushinda katika uchaguzi huo licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka vyama vya  upinzani.
Waangalizi wa kikanda katika uchaguzi huo, wanasema wameridhishwa na maandalizi ya zoezi zima la upigaji kura. Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kati ya Edgar Lungu anayegombea nafasi hiyo kupitia chama tawala na mpinzani wake HAKAINDE Hichilema kutoka United Party for National Development.
Wagombea wote katika nafasi hiyo ya Urais wakati wakijinadi wameahidi kuimarisha mfumo wa elimu nchini humo, kutengeneza ajira. Huku wapiga kura nao wakitumaini kuwa wanasiasa hao watatimiza ahadi zao.
Hata hivyo mshindi katika uchaguzi huo wa leo atatumikia kipindi cha miezi 18 iliyobakia, katika awamu iliyobaki, aliyoiacha marehemu Michael Sata, wakati nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwakani 2016.
Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 12 kamili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni. Tume ya Uchaguzi nchini Zambia imesema zoezi la uhesabuji kura, linatarajiwa kuanza muda mfupi tu baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika, huku matokeo yakitarajiwa kutangazwa katika kipindi cha saa 48.

clouds stream