Wednesday 7 January 2015

AL SHABAAB WAWAUA WAPELELEZI WA MAREKANI ?

AL SHABAAB WAWAUA WAPELELEZI WA MAREKANI ?


Wapiganaji wa kundi la Alshabaab kutoka Somalia wanasema kuwa wamewaua watu wanne wanaodaiwa kuwa wapelelezi wa Marekani, Ethiopia na serikali ya Somalia.
Wpelelezi hao  ambao ni  Wanne,  wanadaiwa kupigwa risasi katika mji wa Baradhere siku ya jumanne baada ya jaji mmoja wa Alshabaab kuwapata na hatia ya kuwaunga mkono wapelelezi wa CIA na mashirika yanayokabiliana na kundi hilo.
Wiki iliyopita maafisa wa Somalia wanasema kuwa shambulizi moja la ndege lililotekelezwa na Marekani lilimuua kiongozi wa ujasusi wa Alshabaab Abdishakur Tahlil.

clouds stream