Friday 16 January 2015

Simeone apagawa na kiwango cha Torres akiichapa Real Madrid 2

Simeone apagawa na kiwango cha Torres akiichapa Real Madrid 2

Kocha mkuu wa klabu ya  Atletico Madrid, Diego Simeone akimpongeza  Fernando Torres kwa kazi aliyoifanya jana
Kocha mkuu wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone akimpongeza Fernando Torres kwa kazi aliyoifanya jana
Kocha mkuu wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone amesema Fernando Torres amerejea kuwa ”mwanaume” baada ya mshambuliaji huyo kufunga magoli yake ya kwanza tangu alipojiunga na Atletico madrid.
Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Torres alijiunga na Liverpool mwaka 2007.
Torres alijiunga na Atletico mwanzoni mwa mwezi huu na aliifungia klabu hiyo magoli mawili katika dimba la Bernabeo na kutoka sare ya mabao 2-2 ilipokutana na Real Madrid katika michuano ya Copa del rey.
Torres naye ameonesha furaha yake na kushukuru wapenzi wake kwa kumuunga mkono.

clouds stream