Friday 16 January 2015

Urais 2015: Ukawa yajipanga kuingia Ikulu

Urais 2015: Ukawa yajipanga kuingia Ikulu


Viongozi wanaounda umoja wa katiba ya wananchi Ukawa.
Viongozi wanaounda umoja wa katiba ya wananchi Ukawa.
Umoja wa katiba ya Wananchi Ukawa unatarajia  kufanya vikao   kwa lengo la kuteua majina ya wagombea ambao watashindanishwa ndani ya umoja huo na  litapatikana jina la mgombea urais mmoja ambaye atatangazwa  rasmi kabla ya mwezi machi mwaka huu. Mgombea huyo atauwakilisha Ukawa kupambana na mgombea kutoka chama tawala cha Mapinduzi (CCM).
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama cha NCCR – Mageuzi James Mbatia amesema kuwa Ukawa wanataria kufanya kikao jumanne januari 20  ambapo kutakuwa na ajenda nyingine lakini: “Suala la kupata wagombea nalo huenda likajadiliwa.
Ameongeza kuwa  ajenda nyingine  ni mwongozo wa Ukawa, kura ya maoni ya Katiba, changamoto za uandikishaji wa daftari la wapigakura, hali ya uchumi na tathmini ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliomalizika Desemba mwaka jana.
Mwenyikiti huyo  pia amesisitiza kuwa  watajadili ajenda hizo ili kuhakikisha wanatafuta majibu ya changamoto zilizopo kwa sasa.
Kwa upande  mwingine kikao hicho kikatoa majibu ni nani ataingia katika kinyang’anyiro cha kugombea urais kufuatia kutokuwepo kwa wanasiasa waliojitangaza kutoka umoja huo, huku chama cha Mapinduzi  makada mbalimbali wakijitangaza kuwa na nia ya kuwania nafasi ya urais mwaka 2015.
Kwa upande mwingine makada   wanaotajwa kuwania urais 2015 ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Prof Anna Tibaijuka,Waziri wa Katiba, Asha-Rose Migiro. Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja. Januari Makamba pamoja na Waziri Lazaro  Nyalandu.

clouds stream