Monday 19 January 2015

Majambazi 40 wateka mabasi 6, wapora kila kitu hadi soksi

Majambazi 40 wateka mabasi 6, wapora kila kitu hadi soksi


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
Majambazi takribani 40 wameteka mabasi 6 ya abiria yanayofanya safari zake kutoka jiji la Arusha kwenda Nairobi nchini Kenya  ambapo wamevamia mabasi 6 na kuwapora abiria hao kila kitu hadi soksi.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi jijini Arusha wamesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana eneo la Mbuga Nyeupe wilayani Longido ambapo majambazi yapatayo 40 yaliweka mawe barabarani na kuamuru abiria wote kushuka chini ambapo waliwapora kila kitu  walichokuwa nacho.
Naye Dereve wa basi aliyekuwepo katika sakata hilo anayeendesha  basi la Perfect Trans, Joseph John alisema majambazi hayo yalikuwa na silaha za jadi ikiwemo mashoka, mapanga na sime ambapo waliteka mabasi hayo majira ya saa nane usiku.
Katika hali ya kushangaza dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jabir Athumani alisema baadhi ya majambazi yalikuwa yakiita majina ya baadhi ya watu na kuwaamuru kutoa fedha walizokuwa nazo suala lilipelekea kuhisi kwamba huenda kundi la majambazi hoa ni kubwa zaidi.
Kufuatia tukio hilo madereva na abiria wamelitaka jeshi la Polisi mkoani humo kurudisha doria katika barabara hizo ili kuepusha matukio ya abiria kuporwa mali zao.

clouds stream