Wednesday 21 January 2015

Mvua yakwamisha upigaji kura Zambia

Mvua yakwamisha upigaji kura Zambia

Hali mbaya ya hewa yakwamisha upigaji kura nchini Zambia.
Hali mbaya ya hewa yakwamisha upigaji kura nchini Zambia.
Hali mbaya ya hewa inadaiwa kukwamisha shughuli za upigaji kura nchini Zambia. Vituo vingi vya kupigia kura vimekabiliwa na chnagamoto ya mvua na hivyo kushindwa kupiga kura ambapo uchaguzi unaendelea leo.
Vituo hamsini na moja vitapiga kura hii leo na  ambapo mvua kubwa  iliyonyesha nchi nzima ya Zambia imesababisha kucheleweshwa kwa karatasi za kupigia kura ni sababu zilizotajwa kusababisha wananchi wa Zambia kutopiga kura.
Katika hatua nyingine hali mbaya ya hewa pia huenda ikasababisha hata matokeo ya uchaguzi kutolewa kama ilivyosemwa awali, naye Rafael Phiri, msemaji wa tume ya uchaguzi ya Zambia amethibitisha kuwa endapo yatachelewa sana haitazidi tarehe ishirini na nne mwezi huu.

clouds stream