Friday 23 January 2015

Toure awatoa hofu mashabiki juu ya Ebola

Toure awatoa hofu mashabiki juu ya Ebola

Kolo Toure mchezaji wa Ivory Coast
Kolo Toure mchezaji wa Ivory Coast
Mlinzi wa Ivory Coast Kolo Toure amewataka mashabiki katika michuano ya mataifa ya Afrika nchini Equitorial Guinea kuwa na Subra wanapokaguliwa ugonjwa wa Ebola.
Mashabiki na maafisa wa polisi wamekuwa wakikabiliana kabla ya mechi kadhaa baada ya kucheleweshwa kutokana na upimaji wa Ebola nje ya viwanja vya soka.
”Nadhani mashabiki wanafaa kujua kwamba ni lazima wakaguliwa, Ebola ipo na watu wengi huwa hawaamini wanapofika katika maeneo ambayo hayana watu walioambukiwa”Amesema Kolo Toure.
Wafanyikazi wa Shirika la afya duniani WHO,ambao wanafanya ukaguzi huo wa Ebola wanakutana alhamisi ili kujadiliana kuhusu wasiwasi wa usalama wao baada ya kukabiliana na mashabiki wengine nchini humo.

clouds stream