Monday 19 January 2015

Jangili wa meno ya ndovu kimataifa kizimbani leo

Jangili wa meno ya ndovu kimataifa kizimbani leo


Feisal Mohammed
Mtuhumiwa  wa ujangili barani Afrika Feisal Mohammed.
Kesi ya Feisal Mohammed anayeshukiwa kuwa mlanguzi mkubwa wa Pembe za ndovu Afrika Mashariki inatarajiwa kuendelea hii leo jijini Mombasa. Feisal amekuwa rumande kwa majuma mawili sasa baada ya kunyimwa nafasi ya kuachiliwa kwa dhamana.
Aidha, Feisal Mohammed anatarajiwa kuanza kujitetea mbele ya Mahakama ya Mombasa , dhidi ya mashtaka ya kumiliki na kulangua kilo 314 ya pembe za ndovu zilizopatikana bandarini Kenya.
Mohamed Feisal Ally alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za uwindaji haramu husani mauaji ya Tembo tatizo ambalo ni kubwa  katika ukanda huu wa Afrika Mashariki hasa Kenya na Tanzania ambapo idadi kubwa ya Tembo wamekuwa wakiuawa kila mwaka na kutishia kutoweka kwa viumbe hao.
Mtuhumiwa alikamatwa nchini Tanzania Desemba mwaka jana, miezi sita baada ya kesi yake kuanza, huku upande wa mashtaka ukisema alitorokea huko baada ya kuarifiwa kuwa anatafutwa na Polisi. Feisal Mohammed ametajwa na Polisi wa Kimataifa Interpol kama mkuu wa kikundi sugu kinacholangua pembe za ndovu.

clouds stream