Monday 5 January 2015

KENYA:SHAHIDI KESI YA RUTO ICC APATIKANA AMEKUFA

KENYA:SHAHIDI KESI YA RUTO ICC APATIKANA AMEKUFA

Maafisa wa polisi nchini Kenya wameupata mwili wa shahidi muhimu wa mahakama ya ICC siku chache tu kabla ya kutoa ushahidi wake katika kesi ya Makamu  wa rais katika mahakama hiyo.
Ripoti za vyombo vya habari nchini Kenya zinasema kuwa mwili wa Meshash Yebei ulipatikana karibu na mto zaidi ya wiki moja baada ya kuonekana akibebwa na kuingizwa katika gari moja lisilo na nambari za usajili katika mji wa Eldoret, umbali wa kilomita 200.
Bwana Yebei alitarajiwa kusafiri kuelekea mjini Hague kwa kesi dhidi ya bwana Ruto-makamu wa rais ambaye anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na mashambulizi dhidi ya watu wa jamii ya kikuyu katika makaazi ya wakalenjin huko Rift valley wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi miaka saba iliopita.

clouds stream