Saturday 24 January 2015

Nigeria:Hatuitaji vikosi vya UN kuwakabili Boko Haram

Nigeria:Hatuitaji vikosi vya UN kuwakabili Boko Haram


Vikosi vya usalama vya UN.
Vikosi vya usalama vya UN.
Wanamgambo wa Boko Haram.
Wanamgambo wa Boko Haram.
Licha kundi la wanamgambo wa Boko Haram kuitesa Nigeria, Nchi hiyo imesema haihitaji msaada wa vikosi vya Umoja wa Mataifa kupambana na Boko Haram.
Kwa mujibu wa Mshauri wa maswala ya usalama wa taifa nchini humo  Sambo  Dasuki amesema Nigeria na majirani zake Niger, Chad na Cameroon wanamudu kushughulikia suala la Wanamgambo wa kiislamu.
Dasuki amekiri kuwa Wanamgambo ni tishio kubwa la usalama nchini humo na kusema kuwa takriban asilimia 50 ya Jeshi la Nigeria limepelekwa kaskazini mashariki . Amesema hatua hiyo inaashiria namna Jeshi lilivyolichukulia suaala hili kwa umakini mkubwa.
Wanamgambo wa Boko Haram walianza Operesheni yao mwaka 2009, wakidai kuwa wanataka kuunda taifa la kiislamu. Tangu Serikali ilipotangaza hali ya hatari miezi 20 iliyopita kaskazini mashariki ili kupambana na Wanamgambo, kundi hilo limejiimarisha na sasa linadhibiti miji kadhaa .

clouds stream