Saturday 24 January 2015

Gazeti la The East African lafungiwa nchini Tanzania

Gazeti la The East African lafungiwa nchini Tanzania

Gazet la East African.
Gazet la East African.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia idara ya Habari Maelezo  imetangaza kupiga marufuku  usambazaji wa gazeti hilo  nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi la  na. 5298 la januari 24,2015  limesema kwamba , Mkurugenzi idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene amesema kuwa hatua hiyo  imechukuliwa kufuatia  kutofurahishwa na jinsi gazeti hilo linavyoripoti habari na uchambuzi wake hasa zinazohusu Tanzania.
Mwambene alilituhumu gazeti hilo  kuwa na mtazamo hasi dhidi ya Tanzania. Alitoa mfano wa maoni ya hivi karibuni ambayo yalikosoa msimamo wa Serikali kuhusu waasi wa Rwanda, FDLR walioko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kama mfano wa mtazamo wa gazeti dhidi ya nchi
Mwambene pia alielezea katuni iliyotoka kwenye toleo la wiki hii la The EastAfrican, kuwa ilionyesha kutozingatia utamaduni na kwamba ilionyesha kutomuheshimu Rais.
Katika Barua  iliyotumwa kwa  mwakilishi wa The EastAfrican nchini, uamuzi huo umechukuliwa kwa sababu gazeti hilo “limekuwa likisambazwa nchini bila ya kuwa na usajili, kinyume na kifungu cha 6 cha Sheria ya Magazeti, Namba 3 ya mwaka 1976”.
Uongozi wa Nation Media Group, ambao unamiliki gazeti la The EastAfrican, umeelezea hatua hiyo kuwa ni ya kushangaza na isiyokubalika. Barua hiyo ya Januari 21, 2015 inaagiza kusimamishwa mara moja kwa uchapishaji na usambazaji wa gazeti hilo nchini Tanzania ‘’hadi litakaposajiliwa rasmi na Msajili wa Magazeti, Idara ya Habari’’.
Kabla ya kutolewa kwa barua hiyo, mwakilishi wa gazeti hilo nchini, Christopher Kidanka aliitwa Jumatano na kuhojiwa na mkurugenzi wa Idara ya Habari.
Akizungumzia uamuzi huo wa Serikali, mwenyekiti wa Bodi ya NMG Group, Wilfred Kiboro alisema sababu zilizotolewa na Serikali zinashangaza kwa sababu gazeti hilo limekuwa likisambazwa tangu miaka 20 iliyopita.
Alisema kwamba sababu halisi “ziko sehemu nyingine “ na zinaweza tu kuhusishwa na msimamo wa gazeti hilo, na mengine ya kampuni NMG, limechukua katika kuripoti rushwa, wizi wa mali za umma na utoaji duni wa huduma kwa watu wa Afrika Mashariki.

clouds stream