Wednesday 7 January 2015

SONG ATANGAZA KUSTAAFU

SONG ATANGAZA KUSTAAFU



Kiungo wa Cameroon pamoja na timu ya ligi kuu ya West Ham Alex Song amestaafu rasmi soka la kimataifa kufuatia kuchwa kwenye timu ya Cameroon inayojiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika nchini Guinea ya Ikweta mnamo januari 17.


Song ambaye ajaitwa kwenye timu hiyo ya Cameroon tangu apate kadi nyekundu kwenye mchezo wa makundi ya Kombe la Dunia nchini Brazil, ameamua kuchukua uamuzi wa kustaafu baada kushindwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Cameroon. Uamuzi huo wa Song umetokea baada ya kujitaidi kuwashawishi ili aweze kutumikia nchi yake bila mafanikio na hivyo kuamua pamoja na familia yake kustaafu.

clouds stream