Wednesday 21 January 2015

Sakata la Escrow: Ikulu yatoa tamko dhidi ya Prof. Muhongo

Sakata la Escrow: Ikulu yatoa tamko dhidi ya Prof. Muhongo


Waziri wa Nishati na Madini Prof.Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Prof.Sospeter Muhongo.
Serikali kupitia  kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imewataka watanzania kuvuta subira kuhusiana na kuwekwa kiporo Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter  Muhongo kufuatia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka achukuliwa hatua kuhusiana na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alisema si kweli Rais Kikwete anakwepa kumwajibisha Profesa Muhongo kama watu wengi wanavyodai bali Rais Kikwete anafuata utaratibu unaotakiwa.
Ameongeza kuwa  taratibu za kumwajibisha Profesa Muhongo kama kiongozi wa kisiasa hazifanani na hatua zilizochukuliwa kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Maswi kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Serikali.
Kwa upande wa  ziara za Profesa Muhongo anazoendelea nazo mikoani, Rweyemamu alisema tuhuma hizo hazimzuii kufanya kazi kwa kuwa bado hajaondolewa kwenye nafasi ya uwaziri aliyonayo.
Profesa Muhongo na baadhi ya viongozi wengine wa Serikali wanahusishwa na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Viongozi wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi ambaye amesimamishwa kupisha uchunguzi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema  amejiuzulu na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye tayari uteuzi wake umetenguliwa.
Katika hatua nyingine desemba 22, mwaka jana, Rais Kikwete akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, alisema amemuweka kiporo Profesa Muhongo, atakapopata ufafanuzi na kujiridhisha, atachukua uamuzi.

clouds stream