Monday 26 January 2015

Guinea ya Ikweta na Congo zavuka Kundi A

Guinea ya Ikweta na Congo zavuka Kundi A


250C470500000578-2925785-image-a-13_1422218345538
Waandaji wa michuano ya mataifa ya Afrika Guinea ya Ikweta wamefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora baada ya kuwachapa Gabon magoli 2-0, kwenye mchezo huo ambao ulikuwa mkali kutokana na kila timu kuwa na nafasi ya kufuzu. Magoli ya Guinea ya Ikweta yamefungwa na Javier Balboa kwenye dakika ya 55 kwa njia ya peanati na goli la pili likifungwa kwenye dakika za majeruhi na Iban Salvador Edu.
250C0C9100000578-2925754-image-a-5_1422215122657
Mchezaji wa Guinea ya Ikweta Javier Balboa akifunga bao kwa njia ya penati
Kwa ushindi huo Guinea ya Ikweta inaungana na Congo ambayo imeifunga Burkina Faso magoli 2-1 huku magoli yakifungwa na  wachezaji Thievy Bifouma na Fabrice Ondama.
Burkina Fasso licha ya kufungwa magoli 2-1 ilishambulia sana lango la Congo huku mshambuliaji wake hatari Bance kulichachafya sana lango la Congo ila bila mafanikio.Congo ambao wanafuzu Kundi A kama washindi wa kundi wakifuatiwa na Guinea ya Ikweta wanasubiria michezo mingine ya makundi ili kujua zitacheza na nchi gani.

clouds stream