Friday 16 January 2015

Nyota wa Ufaransa na PSG kuwania Urais FIFA


Nyota wa Ufaransa na PSG kuwania Urais FIFA



David Ginola anawania Urais wa FIFA
David Ginola anawania Urais wa FIFA
Mchezaji wa zamani waTIMU YA Taifa ya Ufaransa, David Ginola atasimama dhidi ya Sepp Blatter kuwania Urais wa shirikisho la kandanda duniani,FIFA.
Ingawa imetangazwa hivyo hakuna uhakika kama Ginola ataendelea na nia yake.
Anahitaji kuungwa mkono na vyama vitano vya soka na kigezo kingine anapaswa kuwa amejihusisha na soka kwa miaka miwili kati ya mitano iliyopita.
Ginola mwenye miaka 47 , aliichezea Ufaransa, pia club ya nchi hiyo Paris St Germain kabla ya kujiunga na New Castle United kwa kitita cha Pauni milioni 2.5 mwaka 1995.
Zoezi la Uteuzi wa nafasi ya urais wa FIFA litafungwa tarehe 29 mwezi huu.Blatter amekuwa Rais wa FIFA tangu mwaka 1998 anawania muhula wa tano sasa.

clouds stream