Wednesday 7 January 2015

MKIA NDEGE YA AIR ASIA WAPATIKANA LEO

MKIA NDEGE YA AIR ASIA WAPATIKANA LEO



Mkia wa Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyopotea na watu 162 Desemba 28, mwaka jana umepatikana leo katika Bahari ya Java, Indonesia.
Aidha, eneo la mkia ndipo kifaa cha kutunza kumbukumbu za ndege ‘black box’ kinapatikana na upatakianaji wake utasaidia wachunguzi kubaini chanzo cha ndege hiyo kupotea na kisha kuanguka baharini.
Katika hatua nyingine ndege hiyo ilikuwa ikitokea Jiji la Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singaporea. Mpaka sasa miili 40 imeopolewa kutoka baharini.

clouds stream