Monday 26 January 2015

Zitto Kabwe kuibua Kashfa 3 kubwa Bungeni 2015

Zitto Kabwe kuibua Kashfa 3 kubwa Bungeni 2015 

Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe.
Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika mkutano wa vikao vya  Bunge  ulioanza jana mjini Dodoma huenda ukaibua ufisadi mwingine kufuatia ule wa Escrow kuwa bado haujasahaulika.
Katika mkutano huo Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) inatarajia kuibua kashfa  nyingine ambazo ni ufisadi katika gharama za ujenzi wa jengo la watu mashuhuri (VIP) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),misamaha ya kodi  pamoja   na uuzaji wa nyumba ya Bodi ya Korosho.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe amesema kuwa, tayari kamati yake  imepokea ripoti ya ukaguzi huo ambayo inaonyesha ufisadi wa kutisha katika maeneo hayo matatu na mengineyo.
Masuala hayo matatu pia yaliibuka wakati wa vikao vya kamati za Bunge vilivyomalizika Dar es Salaam wiki iliyopita, huku bodi ya korosho ikibanwa kuhusu nyumba yake aliyouziwa Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Silvestry Koka.
Aidha ripoti hiyo inayoonyesha jinsi ufisadi wa kutisha ulivyofanywa katika ujenzi wa jengo la (VIP Lounge) na Serikali inadai ilitumia Sh12 bilioni kulijenga, lakini mthamini wa majengo ya Serikali ameeleza kuwa jengo hilo lina thamani ya Sh 3  bilioni.
Kwa upande wa  misamaha ya kodi, PAC imepokea taarifa kutoka kwa CAG ikionyesha kuwa misamaha hiyo iliyokuwa imefikia Sh1.5 trilioni mpaka Juni 2013, lakini baada ya mwaka moja misamaha hiyo imeongezeka hadi Sh1.8 trilioni mpaka Juni 2014.
Mtandao wa Hivisasa utaendelea kukujulisha kila kinachoendelea Bungeni mjini Dodoma katika vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

clouds stream