Wednesday 21 January 2015

Azam yaichapa Kagera Sugar 3-1CCM Kirumba

Azam yaichapa Kagera Sugar 3-1CCM Kirumba


Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangilia ushindi wao.
Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangilia ushindi wao.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara, Azam FC, leo imefanikiwakuibuka na ushindi mnono wa bao 3-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Katika Mtanange huo Mshambuliaji wa Azam Raia wa Burundi, Didier Kavumbagu, ameendelea kuwika baada ya kufanikiwa kuifungia timu yake bao 2 kwenye ushindi wa bao 3-1.
Kavumbagu amefunga bao lake la kwanza kupitia krosi ya Kipre Tchtche dakika ya 36 na bao la pili dakika ya 64 kufatia kona ya Erasto Nyoni.
Mshambuliaji Kipre Tchetche ndie alikuwa wa kwanza kuiandikia Azam Bao la kwanza katika mchezo huo kunako dakika ya 20 huku Kagera Sugar wakipata bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Rashidi Mandawa kunako dakika ya 52.
Maboa hayo mawili ya Kavumbagu yanamfanya mchezaji huyo azidikujiweka pazuri kuwania kiatu cha ufungaji bora wa ligi kwa kufikisha goli 6 huku wengine wakiwa na mabao manne kwa matatu.
Azam FC watakuwa na kibarua cha kucheza na Simba SC siku ya jumamosi Januari 25, wiki hii katika Uwanja wa Taifa kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara.

clouds stream