Thursday 15 January 2015

Vigogo Sakata la Escrow kufikishwa kamati ya maadili

Vigogo Sakata la Escrow kufikishwa kamati ya maadili


Mbunge mteule wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
Mbunge mteule wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
Sakata ya la Akaunti ya Tegeta Escrow linazidi kuchukua sura mpya  baada ya kamati Kuu ya CCM kuamua viongozi hao ambao ni  Andrew Chenge, William Ngeleja Na Profesa Anna Tibaijuka wafikishwe Kamati ya Maadili ya chama ili kujadiliwa.
Kwa mujibu wa Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Festus Limbu alisema suala la Chenge linasubiri uamuzi utakaotolewa na Spika wa Bunge, Anne Makinda. “Kamati imeamua kwa busara Chenge akae pembeni na makamu mwenyekiti aongoze vikao huku ikisubiri hatua atakazozichukua Spika.
Ameongeza kuwa awali, walitakiwa kuachia ngazi na kamati zao katika mabano ni Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala), Chenge (Bajeti) na Victor Mwambalaswa (Nishati na Madini).
Katika hatua nyingine kikao cha 16 na 17 cha Bunge kiliazimia kuwa kamati husika za kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka  kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge unaoanza Januari 27, kuwavua nyadhifa zao wenyeviti tajwa wa kamati husika.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Ngeleja alisema anaendelea na madaraka yake, kwa kuwa hatua iliyopo sasa ni ya uchunguzi.
Kwa upande mwingine kikao cha kamati kuu CCM kilichoketi jana visiwani Zanzibar kintarajiwa kutoa majibu  kuhusiana na  hatua dhidi vigogo wanao tuhumiwa  kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma.

clouds stream