Wednesday 21 January 2015

Majambazi yavamia kituo cha Polisi, yaua polisi na kupora silaha

Majambazi yavamia kituo cha Polisi, yaua polisi na kupora silaha


Mfano wa silaha zilizoporwa katika kituo cha polisi mkoani Pwani.
Mfano wa silaha zilizoporwa katika kituo cha polisi mkoani Pwani.
Pwani, majambazi waliokuwa wamejihami  na silaha wamevamia katika kituo cha Polisi cha Ikwiri, Rufiji Mkoani  Pwani ambapo inadaiwa wameua askari polisi wawili  pamoja na kupora silaha zilizokuwemo katika kituo hicho.
Aidha, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo. Askari waliopoteza maisha ni Cop Edgar aliyafariki kwa kukatwa mapanga  pamoja na Judith aliyepigwa risasi upande wa kushoto. Silaha zilizoporwa ni  Smg 2, Sar2, Shortgun 1, silaha zingine  pamoja na mabomu ya mchozi na  takribani  risasi 60 za bunduki  aina ya SMG.
Kwa mujibu wa mwananchi mmoja (jina limehifadhiwa) amesema kwamba  leo asubuhi kuna makundi ya watu yamekusanyika katika eneo hilo ambapo jeshi la Polisi lipo katika harakati ya kusaka waliotenda tukio hilo.
Mtandao wa Hivisasa utakujulisha zaidi kuhusiana na  tukio hilo, endelea kuwa nasi.

clouds stream