Thursday 29 January 2015

Majanga yaikumba Tunduru, Mvua yaezua nyumba 51

Majanga yaikumba Tunduru, Mvua yaezua nyumba 51


Zaidi ya nyumba zakosa makazi wilayani Tunduru.
Zaidi ya nyumba zakosa makazi wilayani Tunduru.
Wilayani Tunduru  mkoani  Ruvuma, hali sio shwari   katika kijiji cha Sisi kwa Sisi tarafa ya Mlingotini  kufuatia  mvua kuezua nyumba 51 za makazi ya wananchi. Mvua hiyo  iliyoambatana na upepo mkali imeharibu zaidi ya nyumba 51, wananchi wa kaya zaidi ya 25 wakikosa kabisa sehemu ya  kuishi.
Akizungumzia tukio hilo  mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande  Nalicho amesema tukio hilo la mvua kubwa kunyesha ikiambatana na upepo mkali limetokea Januari 27 mwaka huu majira ya kuanzia saa nane mpaka saa kumi mchana.
Ameongeza kuwa baraza la ulinzi na usalama la wilaya hiyo limejielekeza kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kwenda kujionea hali halisi ilivyo ambayo ameielezea kuwa ni mbaya kwa sababu mbali ya nyumba hizo kuezuliwa, zilizo nyingi zimedondoka kwa sababu ya upepo mkali ulioambatana na mvua hiyo.
Kati ya nyumba hizo 51 zipo nyumba zilizokuwa zimeezekwa bati ikiwemo ofisi ya kijiji pamoja na ghala la mazao ya chakula huku nyumba mbili zilizoezekwa kwa nyasi nazo zimeezuliwa na kudondoka.
Katika hatua nyingine  amewaomba wananchi kuzisaidia kaya zilizoathiriwa huku serikali  ikiendelea kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi hao. Hata hivyo amesema kuwa  hadi sasa  hasara iliyopatikana bado haijafahamika.

clouds stream