Thursday 15 January 2015

Uzalendo wamshinda Nahodha wa ‘Azam’, aruka kushangilia Simba

Uzalendo wamshinda Nahodha wa ‘Azam’, aruka kushangilia Simba


Nahodha akijurusha na mashsbiki wa Simba ndani ya Boti ya Kilimanjaro IV leo asubuhi katika bandari ya Zanzibar.
Nahodha akijurusha na mashsbiki wa Simba ndani ya Boti ya Kilimanjaro IV inayomilikiwa na Azam Kampuni mama ya Klabu ya Azam FC, Jumatano asubuhi katika bandari ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange Kaburu akicheza na mashabiki wa Simba nadani ya Boti leo asubuhi.
Makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange Kaburu akicheza na mashabiki wa Simba nadani ya Boti leo asubuhi.
Mashabiki wa Simba wakicheza ndani ya Boti
Mashabiki wa Simba wakicheza ndani ya Boti
Mmoja wa wafanyakazi wa Azam Marine katika boti ya Kilimanjaro IV, leo amejikuta akiweka chini majukumu yake na kuungana na mashabiki wa Simba kwa kusherekea ubingwa walioupata wa kombe la Mapinduzi kwa kuimba na kucheza ngoma ndani ya boti hiyo ikitokea Zanzibar kuelekea Dar es salam.
Mashabiki hao wa Simba walikuwa wakiimba na kucheza ndani ya boti hiyo ambapo mfanyakazi huyo ambaye anadaiwa kuwa ni nahodha ghafla akajiunga na kikundi hicho cha ushangiliaji na kuanza kucheza kwa furaha kubwa.
Haikuchukua muda mrefu naye Makamu wa Rais wa Klabu hiyo Geoffrey Nyange Kaburu akaingia ndani ya boti hiyo lakini alipokutana ha shamla shamla hizo pia akaungana na mashabiki na kucheza kwa furaha kubwa.

clouds stream