Thursday 29 January 2015

Netanyahu ang’aka kisa kushambuliwa majeshi ya Israel

Netanyahu ang’aka kisa kushambuliwa majeshi ya Israel


Benjamini Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel
Benjamini Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu  amesema  wote  waliohusika na mashambulizi dhidi ya msafara wa majeshi ya Israel watalipa gharama ya waliyoyafanya.
Israel imesema wanajeshi wake wawili waliuawa na wengine saba kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na Hezbollah katika mpaka kati Lebanon na Israel. Mara tu baada ya shambulio lililosababisha wanajeshi hao wawili kuuawa,Israel ilijibu mapigo kwa kufyatua makombora kwenda Lebanon.
Nayo majeshi ya Kulinda amani ya Umoja wa mataifa nchini Lebanon limesema mwanajeshi wao mmoja aliuawa.
Akitoa onyo dhidi ya walihusika na shambulizi hilo Netanyau amesema wote waliohusika lazima wawajibike. Kwa nyakati fulani Iran kupitia Hezbollah imekuwa ikijaribu kuanzisha mashambulizi ya kigaidi dhidi yetu kutoka katika milima ya Golan.
“ Serikali ya Lebanon na utawala wa Rais wa Syria Rais Bashar una utahusika na matokeo yoyote kutokana na mashambulizi yanayoanzisa kutoka kwenye mipaka ya nchi yake dhidi ya taifa la Israel. Kwa matukio yote haya mpango wetu ni kulilinda taifa la Israel. Tunachozingatia ni usalama wa taifa la Israel na watu wake. Ndio maana tutachukua hatua na tataendelea kuchukua hatua.”Amesema Netanyahu.
Nayo Hezbollaha kwa upande wake imekiri kufanya shambulio hilo kwenye msafara wa majeshi ya Israel kwenye mpaka kati ya Lebanona Israel. Hezbollah imesema shambulio hilo ni majibu ya mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israel siku kumi zilizopita ambayo yaliua Jenerali wa Iran na wapiganaji sita wa Hezbollah katika mji wa Queneitra nchini Syria.

clouds stream