Wednesday 21 January 2015

Wanakijiji waua Mamba 2 ziwa Victoria

Wanakijiji waua Mamba 2 ziwa Victoria


Aliyeketi nyuma ni mzee alifanikisha kuuawa mamba hao
Aliyeketi nyuma ni mzee alifanikisha kuuawa mamba hao
Mmoja wa kijana akifurahi  mara baada ya kuuawa mamba hao.
Mmoja wa kijana akifurahi mara baada ya kuuawa mamba hao.
Wananchi wenye hasira kali  katika kijiji cha  Kome- Mchangani wilayani Sengerema mkoani Mwanza, hivi karibuni wamechanga  pesa   ili kufanikisha  kuuawa  mamba wawili wanaodaiwa kusababisha vifo vya watu wawili.
Akizungumza na Mwandishi wetu shuhuda aliyeshuhudia tukio hilo amesema kwamba mamba  walio uawa  walikuwa ni wawili  ambapo  walikuwa wanaonekana  sana katika  katika kingo za Ziwa Victoria katika  kijijini  hicho. Mtu aliyeua  mamba  hao anadaiwa kutumia mbinu zake kuwatega mamba hao na hatimaye kuwaua.
Ameongeza kuwa   mamba hao  walikuwa hatari kwa binadamu suala lilipelekea vifo vya watu wawili huku shughuli  za kiuchumi zinazohusisha uvuvi kukwama kutokana na kuhofia maisha yao.
Katika hatu nyingine wanakiji katika kijiji hicho wameilaumu serikali ya kijiji hicho kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya mamba hao.

clouds stream