Wednesday 21 January 2015

Zambia: Tume yasitisha matokeo ya uchaguzi

Zambia: Tume yasitisha matokeo ya uchaguzi


Wapiga kura waendelea na zoezi la upigaji kura Zambia.
Wapiga kura waendelea na zoezi la upigaji kura Zambia.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Zambia, Bi Irene Mambilima jana alisitisha zoezi la kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu akisema tume imefanya hivyo ili vituo vingine 51 navyo vikamilishe utaratibu wa kupiga kura leo.
Hata hivyo Bi Mambilima alikabiliwa na watu wenye ghadhabu wakitaka Tume ya Uchaguzi iendelee kutoa matokeo ya chama kilichoshinda maana tume hiyo ilikuwa tayari imeshatangaza matokeo ya majimbo 14.
Hata hivyo mwenyekiti huyo wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia amesisitiza kuwa uamuzi huo una manufaa kwa wadau wote, ili kutenda haki. Uchaguzi wa rais nchini Zambia unafanyika kufuatia kifo cha rais Michael Sata, aliyefariki dunia mwaka jana.

clouds stream