Thursday 15 January 2015

Mvua yaleta maafa Msumbiji, watoto wasombwa na maji

Mvua yaleta maafa Msumbiji, watoto wasombwa na maji


Mvua  yaleta maafa msumbiji.
Mvua yaleta maafa msumbiji.
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Msumbiji zimesababisha maafa makubwa ambapo watu kadhaa wamefariki na wengine kupoteza makazi yao.
Serikali ya Msumbiji imetoa tahadhari ya hali ya juu kwenye eneo la kaskazini na katikati mwa nchi hiyo kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua hizo.
Hadi sasa watoto 18 hawajuliani walipo na kuna taarifa watu kadhaa wamesombwa na maji yaliyokuwa yakitiririka katika mto mmoja.
Mawasiliano ya barabara inayounganisha eneo la kati na kaskazini mwa nchi hiyo yameharibika.

clouds stream