Friday 23 January 2015

Taifa Stars imeshindwa kutamba kwa Rwanda, yatoka sare 1-1.

Taifa Stars imeshindwa kutamba kwa Rwanda, yatoka sare 1-1.


Kikosi cha Taifa Stars Maboresho.
Kikosi cha Taifa Stars Maboresho.
Timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu, Taifa Stars Maboresho, leo imeshindwa kutamba mbele ya wageni wao Rwanda ‘Amavubi’, katika mchezo ambao umechezwa jioni hii katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kunako mchezo huo Rwanda ndio walianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wake Mgiraneza kabla ya Tanzania kusawazisha kupitia kwa Kelvin Friday ambaye aliunganisha mpira kutoka kwa Simon Msuva.
Kikosi hicho cha Stars kesho kinatarajia kuondoka jijini humo na wachezaji kurudi kujiunga na timu zao ambapo wengine wanasubiliwa kunako ligi kuu.

clouds stream