Wednesday 21 January 2015

Samatta atikisa Ulaya, Rage awaandaa Simba kupokea Madola ya Usajili wake

Samatta atikisa Ulaya, Rage awaandaa Simba kupokea Madola ya Usajili wake

Mbwana Samatta akiwania mpira katika mazoezi na klabuya CSKA MOSCOW ambayo kwa sasa ipo Hispania kambi.

picha Mbwana akifanya vitu vyake mazoezini na kikosi cha CSK MOSCOW ya Urusi
Mbwana Samatta akiwania mpira katika mazoezi na klabuya CSKA MOSCOW ambayo kwa sasa ipo Hispania kambi.
Mbwana Samatta akiwania mpira katika mazoezi na klabuya CSKA MOSCOW ambayo kwa sasa ipo Hispania kambi.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe, kwa sasa yupo nchini Hispania akifanya majaribio na klabu ya CSKA MOSCOW ya Urusi ambapo jana alifanikiwa kuifungia mabao mawili katika mchezo wa kirafiki.
Kufatia hatua hiyo ya Samatta kuwasha taa ya kijani kuelekea Ulaya, Mwandishi wetu amefanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Mh. Ismail Aden Rage na kusema kuwa, WanaSimba wajiandae kupokea pesa za kutosha endapo mchezaji huyo atasajiliwa huko Ulaya.
Rage amesema kuwa wakati Samatta anasajiliwa TP Mazembe mwaka 2011 kulikuwa na kipengele kwenye mkataba ambacho kinadai kuwa akiuzwa sehemu nyingine basi Simba watapata mgao wa asilimia 30 za Usajili huo.
“Kwanza nampongeza sana huyu kijana wetu, tumuombee aweze kupata nafasi, Viongozi wasijisahau kabisa, Akisajiliwa tu basi Simba itapata mgao wa asilimia 30 kutoka katika pesa za Usajili, hii ipo kwenye mkataba ambao tulisaini na TP Mazembe, Mbona hapa Simba itapata pesa ndefu kuliko hata ile ya Okwi” Amesema Mh. Ismail Aden Rage, Mbunge wa Tabora mjini.
Samatta aliondoka nchini mwishoni mwa wiki kuelekea Hispania kufanya mazungumzo na moja ya timu ya huko inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’, lakini neema ikamdondokea ambapo CSKA waliokuwa wanamuwinda kwa muda mrefu wakaona ndio muda wao wa kumjaribu kitu ambacho kimeonyesha matumaini baada ya kumpa siku tatu lakini wakaona hazitoshi wakamuongezea nyingine nne yaani wiki nzima.
Mbali na CSKA MOSCOW ya Urusi kuhitaji huduma ya Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Simba ya Jijini Dar es salaam, pia timu za Hispania, Uswisi na Italia, zinamvutia kasi mchezaji huyo ikiwemo Inter Milan ya Italia.
Endapo Samatta atafanikiwa kujiunga na matajiri hao wa Urusi, anaweza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na kuwafikia wachezaji wengine wa Afrika Mashariki kutoka Kenya, Mackdonald Mariga (wakati akiwa Inter Milan) na Victor Wanyama (wakati akiwa Celtic).

clouds stream