Sunday 25 January 2015

Simba, Azam hakuna mbabe, zatoka sare

Simba, Azam hakuna mbabe, zatoka  sare


Wachezaji wa Simba Ramadhan Singano na Dan Sserunkuma wakimpongeza Emanuel Okwi baada ya kufunga bao lake
Wachezaji wa Simba Ramadhan Singano na Dan Sserunkuma wakimpongeza Emanuel Okwi baada ya kufunga bao lake
Kapteni wa Azam FC John Bocco akimpongeza mchezaji mwenzake Kipre Tchetche kwa bao alilofunga huku wakicheza.
Kapteni wa Azam FC John Bocco akimpongeza mchezaji mwenzake Kipre Tchetche kwa bao alilofunga huku wakicheza.
Mchezo kati ya Simba na Azam FC uliokuwa unapigwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, umemalizika kwa timu hizo kufungana bao moja moja na kufanya kugawana pointi licha ya wachezaji kupoteza nafasi za wazi kwa kila timu.
Simba ndio walikuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa Emanuel Okwi dakika ya 19 kipindi cha kwanza ambapo alipiga mpira ambao uliingia moja kwa moja golini, na kufanya mchezo huo kumalizika kwa dakika 45 za kwanza vijana hao wa Msimbazi wakiongoza kwa bao hilo.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Azam wakisaka bao la kusawazisha na ilipofika dakika ya 57 Mshambuliaji wa Azam FC Kipre Herman Tchetche akaiandikia bao la kusawazisha timu yake kabla kocho Joseph Omog haja mtoa na kuingia Kelvin Friday.
Kwa bahati mbaya Mashabiki wa Simba hadi mchezo unamalizika walikuwa katika hari ya Udhuni baada ya Nyota wao Emanuel Okwi kutolewa uwanjani na Madaktari akiwa hajitambui baada ya kuzimia alipogongana na beki wa Azam, Agrey Morris,Lakini amekimbizwa hosptala kwa matibabu zaidi.

clouds stream