Friday 23 January 2015

UKAWA yawataka wananchi kususia kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa

UKAWA yawataka wananchi kususia kura ya maoni


Viongozi wa Ukawa katika mkutano na Waandishi wa Habari.
Viongozi wa Ukawa katika mkutano na Waandishi wa Habari.
Viongozi wakuu wa vyama vinavyuounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA  leo  wamewataka wananchi wanaowaunga mkono umoja huo kutoshiriki katika zoezi la kupiga kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi aprili mwaka huu kutokana na mchakato mzima wa kupatikana kwa katiba hiyo inayopendekezwa ulikuwa batili.
Kwa mujibu wa  Prof  Ibrahimu Lipumba  amesema UKAWA hawawezi kushiriki katika kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa ambayo haijapatikana katika misingi ya kidemokrasia pamoja na ukiukwaji wa makubaliano ambapo awali kupitia kituo cha demokrasia-TDC- walikubaliana na Mhe.Rais kwamba zoezi hilo lifanyike baada ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge jambo ambalo halikutekelezwa.
Naye, mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema mpaka sasa ziko katiba pendekezwa zaidi ya nne mitaani jambo linalozidi kuwachanganya wananchi. Amesisitiza kuwa haiwezekani daftari ya kudumu la wapiga kuwa tayari kabla ya mwezi aprili.
Kwa upande wake James Mbatia ameshitushwa na zoezi la kupiga kura ya maoni ya katiba pendekezwa linalotarajiwa kufanyia mapema mwezi aprili wakati wananchi hawajapata elimu ya kutosha, sambamba na viongozi wa vyama kutopatiwa katiba inayopendekezwa na kusisitiza  kuwa umoja huo sasa umejielekeza zaidi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu.

clouds stream