Thursday 12 February 2015

Afrika kusini: Ngumi zapigwa Bungeni, upinzani watimuliwa

Afrika kusini: Ngumi zapigwa Bungeni, upinzani watimuliwa

Wanbunge wakizichapa ngumi kavukavu Bungeni.
Wanbunge wakizichapa ngumi kavukavu Bungeni.
Jumba linalodaiwa kuwa ni Rais Zuma.
Jumba linalodaiwa kuwa ni Rais Zuma.
Bunge la Afrika kusini liligeuka kuwa uwanja wa vita ambapo wabunge wa upinzani ilifikia hatua ya kuvutana mashati na maafisa wa usalama na kufanya wabunge wa upinzani wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) wakiongozwa na Julias Malema kutolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa nguvu na baadae wabunge wengine wa upanzani nao wakatoka nje ya ukumbi.
Sakata hilo lilizuka wakati Rais wa nchi hio Jacob Zuma alipokuwa akilihutubia taifa na kuulizwa maswali na wabunge wa chama cha EFF kinachoongozwa na Julius Malema wakitaka kujua ni lini atarejesha pesa zilizojengea jumba lake la kifahari la Nkandla.
Kwa upande mwingine Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameingia kwenye kashfa ya ufujaji wa fedha za Serikali yake kutokana na   kufanya ukarabati wa jumba lake la kifahari kwa gharama ya dola milioni 25 sawa na zaidi ya Bilioni 3 za Kitanzania.
Taarifa za nchini humo zinaeleza kuwa, ukarabati huo wa jumba lake gharama zake zote zinatarajiwa kulipwa na serikali. Kufuatia hatua hiyo, uchunguzi umeanza kuhusu ukarabati huo ambao ni nyumba yake binafsi  na sio mali ya umma.

clouds stream