Monday 16 February 2015

Jeshi lafanikiwa kuwaondoa Boko Haram Gombe


Jeshi lafanikiwa kuwaondoa Boko Haram Gombe



Wanamgambo wa Boko Haram.
Jeshi la nchini Nigeria  limefanikiwa  kuwaondoa wapiganaji Waislamu wa Boko Haram  katika mji wa Gombe kaskazini-mashariki mwa Nigeria baada ya mapambano makali.
Aidha, maofisa wa Jeshi la Nigeria  wanasema wapiganaji wamerejeshwa nyuma, lakini ripoti nyingine zinasema kuwa wapiganaji hao waliondoka kwa hiari yao.
Boko Haram waliingia Jumamosi asubuhi katika vitongoje vya Gombe baada ya kushambulia mji jirani wa Dadin Kowa.
Wapiganaji hao wamewahi kufanya mashambulio ya kujitolea mhanga katika mji wa Gombe, lakini hawakuuteka  mji huo.
Katika hatua nyingine Nigeria ilitarajiwa kufanya uchaguzi tarehe 14 Februari, lakini umeahirishwa kwa wiki sita kwa sababu ya wasiwasi  wa usalama kutokana na mashambulizi ya wanamgambo wa Boko Haram.

clouds stream