Thursday 19 February 2015

Mauaji ya Albino Geita Baba mzazi awekwa Lupango

Mauaji ya Albino Geita Baba mzazi awekwa Lupango


Jeshi la Polisi mkonai Geita  Polisi linamshikilia  baba mzazi wa mtoto  aliyeuawa  anayefahamika kama Bahati Misalaba  mkazi wa kitongoji cha Mapinduzi katika kijiji cha Lumasa, wilayani Chato, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Joseph Konyo amesema   mtoto Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi (albino), aliyetekwa katika Kijiji cha Ilelema wilayani Chato katika Mkoa wa Geita,  mwili wake umekutwa ukiwa umefukiwa huku umenyofolewa miguu na mikono.
Ameongeza kuwa katika tukio hilo, watekaji  waliokuwa na silaha mbalimbali za jadi,  walimjeruhi  pia Ester Bahati (30), ambaye ni mama wa mtoto ambaye  kwa  sasa  amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Ametoa mwito kwa wananchi kutoruhusu tukio lingine la namna hiyo litokee, badala yake wachukue hatua mapema kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika vya dola viweze kudhibitiwa.

clouds stream