Thursday 19 February 2015

Baloteli aendeleza vituko Liverpool

Baloteli aendeleza vituko Liverpool

Nahodha wa Liverpool Steven Gerald amechukizwa kwa kitendo cha mchezaji mwenzake wa Liverpool Mario Balotelli kumnyang’anya mpira nahodha Jordan Henderson wakati akijiandaa kupiga penati.
Gerard alikasirishwa kwa kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kwa Baloteli kupiga penati ya dakika ya 85 huku anajulikana mpigaji wa penati hiyo ni Jordan Henderson kwenye mchezo wa kombe la Uropa dhidi ya timu ya Besiktas ya Uturuki.
Balotelli alifunga penalti hiyo na kuiwezesha Liverpool kuibuka washindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi ya Uropa unaozishirikisha timu 32 uliochezwa Alhamisi katika uwanja wa Anfield.
Balotelli ana rekodi nzuri kwenye upigaji wa penati katika penati 29 za klabu na timu ya taifa alizopiga amefunga penati 27.
Gerrard amesema: “Henderson ni nahodha na Balotelli kwa kiasi fulani alionyesha kumkosea adabu katika hali hiyo.”
Gerrard ambaye kwa sasa ni majeruhi, alikuwa mchambuzi katika matangazo ya mchezo huo kwenye televisheni ya ITV ya nchini Uingereza.
Pia Gerard alimsifu kwa kufunga penati hiyo hila si jambo zuri wachezaji kuzozana wakati mpigaji wa penati anajulikana, Kocha wa timu hiyo Brendan Rodgers akuzungumza jambo lolote kuhusu jambo hilo.

clouds stream