Tuesday 17 February 2015

Misri yaomba msaada UN kukabiliana na Islamic State

Misri yaomba msaada UN kukabiliana na Islamic State


Rais wa misri Abdel Fatah Al-Sisi ameutaka umoja wa mataifa kuidhinisha hatua za kijeshi za kimataifa dhidi ya kundi la Islamic State pamoja na Jihadi  nchini Libya.
Akizungumza na kituo kimoja cha radio cha Ufaransa ( Europe One) rais Sisi alisema kuwa watu nchini Libya wanataka hatua kali kuchukuliwa ili kuleta usalama na udhabiti nchini mwao. ”Hatutawaruhusu watoto wetu wachinjwe ovyo na hawa magaidi.” Al sisi alisema
Wito wa rais Sisi unakuja siku moja baada ya ndege za kivita za Misri kushambulia ngome za Islamic State kulipiza kisasi kuuawa kwa wamisri wa dhehebu la Coptic nchini Libya siku ya Jumamosi.
Hapo jana , Taarifa kutoka Misri zilisema kuwa, ndege za kijeshi ziliwashambulia wapiganaji wa jihadi nchini Libya kwa mabomu, baada ya kutolewa kwa mkanda wa video ulioonyesha wakristo wa Misri wa madhehebu ya Coptic wakichinjwa.

clouds stream