Friday 13 February 2015

Rais wa Nigeria akana kukwamisha uchaguzi mkuu

Rais wa Nigeria akana kukwamisha uchaguzi mkuu

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
Bango la Kampeni la Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan.
Bango la Kampeni la Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan.
Uchaguzi wa Rais nchini  Nigeria umechukua sura mpya  kufuatia  Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan kukana   kuwa  alishauriwa kuhusu kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais nchini humo siku ya jumamosi.
Inadaiwa kwamba  Maafisa wa uchaguzi walichukua hatua hiyo kufuatia ushauri wa wasiwasi wa maafisa wa usalama kuhusu mashambulizi ya wapiganaji wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Akizungumza kupitia televisheni Rais Goodluck amesema kucheleweshwa kwa uchaguzi kwa kipindi cha wiki moja sio kitu kikubwa.
Kwa upande wa   upinzani umedai kwamba bwana Johnathan alilazimisha uchaguzi huo kucheleweshwa kwa kuwa alikuwa anaogopa kushindwa. Hata hivyo uchaguzi huo umeahirishwa hadi tarehe  28 mwezi machi mwaka huu.
Wakizungumzia uchaguzi huo wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema kuwa  kuwa uchaguzi huo ndio ulio na ushindani mkali tangu uongozi wa kijeshi ulioisha mwaka 1999.

clouds stream