Thursday 12 February 2015

Kova apiga marufuku maandamano ya CUF jijini Dar es salaam kesho

Kova apiga marufuku maandamano ya CUF jijini Dar es salaam kesho

mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana chama cha Wananchi Cuf (JUVICUF)  akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana chama cha Wananchi Cuf (JUVICUF) akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanada maalumu ya Dares salaam Suleiman Kova akipiga marufuku maandamano hayo.
Kamanda wa Polisi wa Kanada maalumu ya Dares salaam Suleiman Kova akipiga marufuku maandamano hayo.
Dar es salaam, Jumuiya ya vijana chama cha Wananchi Cuf (JUVICUF) leo wametangaza kufanya maandamano ya amani kesho ijumaa hata hivyo jeshi la Polisi limepiga maruku maandamano hayo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Hamidu Boban amesema kuwa maandamano hayo yataongozwa na Waziri wa Miundombinu na Uchukuzi Zanzibar Bw. Juma Duni Haji  na  yataanzia maeneo ya Buguruni na kuelekea ofisi za wizara ya Mambo ya ndani na baadae kuelekea tume ya Taifa ya uchaguzi Tanzania.
Lengo la maandamano hayo ni kupinga na kulaani vikali nguvu na uvunjaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la Polisi. Lengo lingine la maandamano hayo ni kufikisha malalamiko yao tume ya uchaguzi kuhusiana na uchache wa siku zilizowekwa za uboreshaji wa Daftrari la kudumu la wapiga kura.
Katika hatua nyingine  Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova amepiga marufuku  maandamano  hayo  na  kusisitiza kuwa maandamano hayo siyo halali na itakuwa ni mbinu ya kuvuruga amani jijini Dares salaam.
Ameongeza kuwa sababu zilizotolewa za kufanya maandamano hayo ni sababu ambazo zinajadilika hata bila maandamano hivyo haoni haja ya kufanya maandamano hayo badala yake watafute njia nyigine ya kuwasilisha malalamiko yao.
Kwa upande mwingine amesisitiza kuwa kutokana na taarifa kuwa vijana hao wa CUF bado wanazidi kuhamasishana  kufanya maandamano ni dhahiri kuwa  lengo lao ni uvunjifu wa amani hivyo basi Polisi watatumia uwezo wao  kuhakikisha kuwa wanazima maandamano hayo.

clouds stream