Thursday 12 February 2015

Nahodha wa meli ya Costa Concordia Bw. Francesco Schettino.

Nahodha meli ya Concordia atupwa jela miaka 16

Nahodha wa meli ya Costa Concordia  Bw. Francesco Schettino.
Nahodha wa meli ya Costa Concordia Bw. Francesco Schettino.
Nahodha wa meli ya Costa Concordia iliyosababisha vifo vya watu watu 32 wakiwemo wafanyakazi wa meli hiyo amehukumiwa kwenda jela.
Kwa mjibu wa hukumu hiyo Nahodha huyo atatumikia kifungo cha miaka 16 jela baada ya kubainika kuwa na makosa ya kuua bila kukusudia.
Francesco Schettino hakuwepo Mahakamani wakati hukumu hiyo ikitolewa. Miaka mitatu iliyopita Meli hiyo ya Costa Concordia iligonga miamba karibu na pwani ya Giglio nchini Italia na kusababisha vifo hivyo.
Kufuatia  hukumu  hiyo Schettino bado ana fursa ya kuweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

clouds stream