Thursday 19 February 2015

Magaidi wengine 4 watiwa mbaroni Tanga

Magaidi wengine 4 watiwa mbaroni Tanga

Tanga, watuhumiwa wengine  wanaodaiwa kuhusiana na makundi ya kigaidi jijini Tanga wamekamatwa kufuatia wananchi kuwafichua  katika mapango waliyojificha  eneo  la amboni jijini Tanga.
Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na viongozi wa jeshi la polisI jijini Tanga  wamesema kwamba baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa  ni wenye asili tofauti wakiwemo wenye asili ya kiarabu huku wengine wakiwa na asili ya kisomali ambao wote kwa pamoja wamekamatwa na wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
Nao  wananchi walioshiriki katika zoezi hilo wakielezea jinsi walivyowadhibiti watuhumiwa ambao walikamatwa kwa nyakati tofauti wakiwa wamechoka katika vichaka vilivyopo pembeni mwa mapango ya maji moto yaliyokuwa yakihifadhi wahalifu yaliyopo kilomita 5 kutoka katika yale mapango ya amboni.
Inadiwa kuwa  kukaa na njaa ndio sababu kuu iliyowafanya kuwakamata kiurahisi kisha kuwapigia simu askari wa jeshi la wananchi kwa lengo la kuwakabidhi watuhumiwa.

clouds stream