Thursday 12 February 2015

SUMATRA, TANESCO waagizwa kushusha bei

SUMATRA, TANESCO waagizwa kushusha bei


Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene.
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene.
Shirika la Umeme Nchini Tanzania (TANESCO) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra)  wametakiwa kutangaza bei mpya  kufuatia  kushuka kwa bei ya mafuta nchini na soko la dunia kwa ujumla.
Akizungumza  baada ya mkutano wa pamoja kati ya wadau na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amezitaka taasisi hizo  kuangalia uwezekano wa kushusha gharama za umeme ili kushuka kwa mafuta kuwaguse moja kwa moja wananchi wa kawaida.
Aidha, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) nayo imetakiwa kuangalia namna itakavyoweza kushusha bei za nauli ili kushuka kwa gharama za mafuta ziendane na unafuu wa maisha kwa wananchi wote.
Waziri Simbachawene  ameiomba Sumatra iweze kuchukua hatua za haraka za kutangaza bei mpya za nauli ambazo zitakuwa chini tofauti na ilivyo sasa.
Kwa upande mwingine bei ya bidhaa za petroli zimekuwa zikishuka bei kutokana na kushuka kwa bei katika soko la dunia ambapo  unafuu umeanza kuonekana kwa watumiaji  mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa.

clouds stream