Friday 13 February 2015

El-Merreikh kutua Dar leo, tayari kuikabili Azam

El-Merreikh kutua Dar leo, tayari kuikabili Azam

Kikosi cha El-Merreikh kinatarajiwa kuwasili leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Azam FC
Kikosi cha El-Merreikh kinatarajiwa kuwasili leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Azam FC
Timu ya El-Merreikh ya Sudan inatarajiwa kuwasili leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuikabili timu ya Azam FC kwenye mchezo wa raundi ya awali wa klabu bingwa Afrika (CAF Champions League) utakaochezwa Jumapili kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.
El-Merreikh inatarajiwa kuwasili majira ya saa saba mchana, timu hiyo ni ni moja ya timu zenye uzoefu mkubwa kwenye michuano mikubwa ya Afrika ukilinganisha na timu ya Azam FC.
Mchezo kati ya Azam na El-Merreikh utachezeshwa na mwamuzi Hassan Mohamed Hagi akisaidiwa na Bashir Abdi Sule na Salah Omar Abubakar wakati mwamuzi wa mezani atakua Kidane Terfe, waamizi wote wanatoka Somalia.
Kwa mara ya mwisho Azam na El-Merreikh zilikutana Agost 20 mwaka jana kwenye robo fainali ya kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda. El-Merreikh wakaibuka na ushindi wa penati 4-3 baada ya kutoka sare ya bila kufungana kweye muda wa kawaida.
Lakini Azam wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara kwa goli 5-2 dhidi ya Mtibwa Sugar kitu ambacho kitawaongezea kujiamini wakati watakapo kabiliana na mabingwa hao kutoka sudan.

clouds stream