Thursday 26 February 2015

Arsenal yashindwa kutamba nyumbani, yakubali kipigo cha 3-1

Arsenal yashindwa kutamba nyumbani, yakubali kipigo cha 3-1


Mshambuliaji wa Monaco Dimitar Berbatov alifunga goli la pili Monaco ikiichapa Arsenal 3-1
Mshambuliaji wa Monaco Dimitar Berbatov alifunga goli la pili Monaco ikiichapa Arsenal 3-1
Matumain ya Arsenal yapo mashakani kwenye michuano ya ligi ya mabigwa Ulaya baada ya kukubali kichapo cha goli 3-1 kutoka kwa Monaco kwenye mechi ya kwanza hatua ya 16 bora mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Emirates.
Geoffrey Kondogbia alliifungia Monaco goli la kuongoza kabla ya mshambuliaji wa zamani wa Tottenham kuongeza goli la pili kipindi cha pili wakati Arsenal wao walishindwa kutumia vyema nafasi zao walizopta.
Olivier Giroud na Danny Welbeck walikosa magoli ili kuirejesha Arsenal kwenye mchezo kabla ya Alex Oxlade –Chamberlain kuifungia timu yake dakika za majeruhi, lakini Ferreira Carrasco akafunga goli la tatu kwa Monaco kwenye dakika za nyongeza za mchezo huo.
Arsenal waliunza vizuri mchezo kwa kumiliki mpira vizuri dakika za mapema za kipindi cha kwanza lakini walishindwa kutumia nafasi hiyo kupata goli, dakika chache baadae Monaco walianza kucheza mpira wa kasi na kuwafanya Arsenal kuwa kwenye wakati mgumu kwa muda mwingi wa mchezo.
Ushindi huo ni wa kwanza kwa klabu ya Monaco kwenye uwanja wa Emirates ambao unawaweka vijana wa mzee Wenger kwenye mazingira magumu ya kufuzu kwa hatua inayofuata ya robo fainali, Arsenal kama watatolewa kwenye hatua hiyo itakua ni mara ya tano mfululizo kutoka kwenye hatua ya 16 bora.
Kwenye mchezo mwaingine uliopigwa huko Ujerumani, wenyeji timu ya Bayern Liverkusen wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Atletico Madrid huku goli pekee la washindi likifungwa na Calhanoglu.

clouds stream